SOLSKJAER: MANCHESTER UNITED ILIKUWA NA PESA ZA KUTOSHA
Msimu wa mpya wa ligi kuu England ukiwa unaanza, kocha wa klabu ya Man United Ole Gunnar Solskjaer amedai klabu yake ilikuwa na uwezo wa kusajili wachezaji zaidi baada ya kuulizwa kama walikuwa na uwezo zaidi kuongeza wachezaji.
Katika dirisha hili Man United imesajili wachezaji watatu pekee kwa jumla ya pauni 145 millioni huku dakika za mwisho wakimuuza mshambuliaji wao Romelu Lukaku kwenda Inter Mila kwa pauni 73 millioni.
.
“ Pesa zipo pindi wachezaji sahihi wanapokuwepo “ ameongea Solskjaer baada ya kuhojiwa kama walikuwa na pesa za kuongeza wachezaji katika kikosi chake.
Kocha huyo amesema kujenga kikosi sio swala la kufanyika kwa haraka bali kwa umakini na taratibu na kuongeza kuwa ana imani na wachezaji waliopo katika kikosi chake cha sasa.