Mtanzania kucheza timu moja na Zlatan
Beki wa zamani wa Yanga SC Abdallah Shaibu Ninja amesaini wa mkopo wa mwaka mmoja katika klabu LA Galaxy ya nchini Marekani akitokea MFK Karvina ya daraja la tatu nchini Czech Republic.
MFK ilimpa mkataba wa miaka minne na sasa wamemtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja LA Galaxy.
LA Galaxy ndio timu anayoichezea mshambuliaji wa zamani wa klabu za Man United, PSG, Barcelona, Inter Milan Zlatan Ibrahimovic