Rais wa Napoli aponda usajili wa Maguire
Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema kama Man United wamemnunua Harry Maguire kwa Pauni Milioni 80, basi beki wao Kalidou Koulibaly ana thamani ya Pauni Milioni 250.
Maguire amejiunga na Man United kutoka Leicester katika majira haya ya kiangazi na kusaini mkataba wa miaka sita huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Man United walikuwa wakihusishwa na kumsajili Koulibaly kwa muda mrefu ambaye kipengele cha kumuuza ilikuwa ni Pauni Milioni 150.