Diego Forlan astaafu soka
Nahodha wa Uruguay Diego Forlan ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 40.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuvichezea vilabu Man United, Villarreal,Atletico Madrid na Inter Milan ametangaza maamuzi yake hayo kupitia mtandao wa Twitter leo.
“ Baada ya miaka 21 nimefanya maamuzi ya kumaliza Career yake yangu kama mchezaji wa soka” Aliandika.