David Ochieng ajiunga na ligi kuu ya Saudi Arabia
Beki wa timu ya Taifa ya Kenya David Ochieng amejiunga na klabu ya Al Nasr ya ligi kuu nchini Saudi Arabia baada ya mkataba wake na AFC Leopards kumalizika mwezi Juni 2019.
Al Nasr imewahi kuchukua ubimgwa wa ligi kuu ya Saudi Arabia mara nane, vikombe viwili vya GCC Champions League, vikombe vitatu vya Saudi Crown Prince, na vikombe sita vya Saudi Kings Cup.