Gavana wa Nairobi kujenga Gym ya wacheza kikapu
Gavana wa jiji Nairobi Mike Sonko ameahidi kujenga jumba la mazoezi (gym) kwa wachezaji wa mpira wa kikapu jijini humo .
Gavana huyo amesema kuwa jiji la Nairobi lipo tayari kukuza vipaji na pia ametangaza kuwa zaidi ya viwanja vinne vya mpira wa kikapu vitajengwa jijini humo. .
“Viwanja vitano zaidi vitajengwa ndani ya Mwiki, Dagoretti, Tena, Mihango na Mukuru kwa njenga ili kuwasha moto wa michezo uliokua umezimika”,alisema sonko.
Haya yote ni baada ya timu ya Kenya ya mpira wa kikapu kushika nafasi ya pili katika mashindano ya inaugural FIBA afrocan basketball tournament yaliyofanyika huko nchini Mali.
Gavana sonko ameipa timu hiyo ya mpira wa kikapu Maarufu Kama “Kenyan Morans”pongezi yake binafsi ya pesa taslimu kiasi cha Ksh Milioni moja (Tsh Milioni 22) Kwa jitihada zao.
Pia alimalizia kwa kusema kwamba michezo mingine Kama vile kuogelea, mpira wa wavu na netiboli hataziacha nyuma .