Bocco ala shavu timu ya Taifa
Nahodha wa Klabu ya Simba SC John Bocco ametauliwa na kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars Ndayiragije Etienne kuwa nahodha wa timu ya Taifa kwa wachezaji wa Ndani.
Bocco atasaidiana na Juma Kaseja, Kelvin Yondan na Erasto Nyoni.
Kikosi hicho cha Taifa Stars kitashuka dimbani Jumapili hii kucheza na Kenya uwanja wa Taifa Dar es salaam katika mchezo wa kuwania kucheza michuano ya CHAN mwakani nchini Cameroon.