Bondia mwingine afariki dunia
Siku kadhaa baada ya bondia Mrusi Dadavesh kufariki sababu ya majeraha ya ngumi, Alhamis hii bondia mwingine Muargentina Hugo Santillan amefariki kutokana na majeraha ya ngumi.
Bondia huyo aliyekuwa na miaka 23 alizimia ulingoni muda mchache baada ya pambano lake la kuwania ubingwa wa Latino Silver Weight dhidi ya Muargentina mwenzake Eduardo Aberu kuisha kwa sare siku ya Jumamosi.
Alipelekwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa dharura ili kuokoa maisha yake lakini juhudi hizo hazikufanikiwa, akafariki dunia jana Alhamisi.