Solskjaer awatoa hofu Mashabiki Man United
Dirisha la usajili Ligi Kuu England linafungwa Agosti 8 siku tatu kabla ya Manchester United hawajacheza mchezo wao wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England 2019/2020 lakini bado mashabiki hawajaona jina kubwa likitua katika kikosi chao.
Kocha mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amewatoa hofu mashabiki wa Manchester United na kueleza kuwa kabla ya dirisha la usajili halijafungwa atakuwa amefanya usajili mpya wa wachezaji wawili au mmoja kwa ajili ya maboresho ya kikosi chake.
.
“Siwezi kusema sana zaidi ya kusema tuna kikosi kizuri kwa sasa tulionao hawa wameunda timu nzuri, mengi yamekuwa yakiandikwa na sisi kuhusishwa na wachezaji wanaofikia 150 katika majira haya ya joto lakini usajili wa mchezaji mmoja au wawili unaweza kutokea pia inawezekana wote wakawa ndani ya Ligi hii au nje chochote kinaweza kutokea” alisema Ole Gunnars Solskjaer
Mashabiki wa Manchester United walitegemea kuona usajili wa nguvu katika timu yao kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 hiyo inatokana na kusuasua msimu uliopita kiasi cha kushindwa kupata matokeo chanya katika michezo yake mitano ya mwisho wa msimu huku wakipoteza michezo mitatu na sare mbili.
Hadi sasa zikiwa zimesalia siku 13 dirisha la usajili kufungwa Manchester United chini ya kocha wao Ole Gunnar Solskjaer wamefanya usajili wa wachezaji wawili pekee Aaron Wan-Bissaka kutoka Crystal Palace na Daniel James kutoka Swansea City, usajili ambao hauwapi amani mashabiki.