Barca yaachana na Meneja wao
Uongozi wa juu wa klabu ya Barcelona leo umethibitisha kuwa wamefikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha mkataba na Meneja Mkuu wao wa Michezo Pep Segura.
Imeripotiwa kuwa Eric Abidal ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa mpira wa miguu wa timu hiyo anatajwa kuwa ndiye atakuwa mrithi wa Segura.
.
“Barcelona na Josep Segura wamefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na klabu, faraja kufanya kazi na Segura na kujitoa kwa muda wote na tunamtakia kila la kheri huko aendako” Taarifa iliyotolewa na Barcelona haijaeleza zaidi sababu za kufikia makubaliano hayo
Hakuna taarifa zaidi zinazoeleza sababu za kufanya mabadiliko hayo ya kumuondoa Pep Segura katika kiti hicho.
Segura alijiunga na Barca mwaka 2015 na alikuwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja.