Tanzania yaporomoka katika viwango vya soka
Tanzania imeshuka katika kwa nafasi 6 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa leo na FIFA leo Julai 25,2019, kutoka nafasi ya 131 na sasa inashika nafasi ya 137.
Katika viwango hivyo Kenya wameshuka kwa nafasi mbili na sasa wapo nafasi ya 107, huku Uganda ambao walifika hatua ya 16 bora katika michuano ya AFCON iliyomalizika hivi karibuni nchini Misri, wamebaki katika nafasi ya 80 waliyokuwa awali.
