Sanamu ya Mo Salah yakosolewa vikali
Sanamu ya mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah imezinduliwa jana nchini Egypt , na kuleta maneno kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Sanamu hiyo iliyozinduliwa kwenye mji wa Sharm-el Sheikh inamuonesha Mo Salah ambaye alikuwa kinara wa magoli katika ligi kuu nchini England msimu uliopita akiwa ameweka pozi la aina yake ya ushangiliaji.
Kazi ya utengenezwaji wa sanamu imefanywa na mwanadada Mmisri Mia Abdel Allah
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamesema mwanadada huyo amemtengeza Salah aonekane kama waimbaji wa miaka ya 1970 Leo Sayer au Art Garfunkel , huku wengine wakimfananisha na Marv wa filamu ya Home Alone
Sanamu hiyo imekumbusha maneno yaliyotokea baada ya sanamu ya Cristiano Ronaldo kuzinduliwa katika uwanja wa ndege wa Madeira, mpaka kupelekea mtengenezaji Emanuel Santos kutengeneza nyingine kufuatia ya mwanzo kutoendana na staa huyo wa Ureno.
Mwanadada huyo, Abdel Allah amesema kuwa alivutiwa kutengeneza sanamu ya mchezaji huyo na kuionesha katika World Youth Forum hapo jana.
Mwanadada huyo amesema kuwa amepokea maoni na ukosoaji wote kwa uzuri na heshima na kuahidi kuwa kazi yake nyingine inakuja na maonesho mengine mwezi kesho.