Simba kucheza na Wazambia Simba Day
Katika kuazimisha siku ya wekundu wa Msimbazi (Simba Day) kikosi cha Simba SC kitashuka Dimbani Agosti 6 mwaka huu dhidi ya Power Dynamos kutoka nchini Zambia.
Kilele cha siku hiyo kitakuwa Agosti 6 na si 8 tena kutokana na ratiba ya Ligi ya klabu Bingwa Afrika kutoka na Klabu hiyo kupangwa kucheza raundi ya awali dhidi ya timu ya UD DO SONGO ya Msumbiji kati ya tarehe Agosti 9-11, ambapo Simba wataanzia ugenini na mechi ya marudiano kuchezwa kati ya Agosti 23,24,na 25.