Apewa zawadi ya kuku baada ya Man of the Match
Achana na yule aliyepewa Sambusa baada ya kufunga Hat Trick. Huko nchini Malawi mchezaji wa Nyasa Big Bullets Hassan Kajoke amepewa kuku na shabiki mmoja kama zawadi ya kuwa mchezaji bora wa mechi.
Katika mechi hiyo ya ligi kuu nchini Malawi waliyocheza dhidi ya Karonga United juzi Jumapili wakishinda kwa goli 5-0, Kajoke alifunga magoli mawili na kuonesha kiwango bora.