Algeria Mabingwa wa Africa
Timu ya Taifa ya Algeria imefanikiwa kuchukua Ubingwa wa michuano ya AFCON 2019 nchini Misri baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Senegal katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Cairo International.
Goli pekee la mechi hii limefungwa na mshambuliaji Baghdad Bounedjah mapema katika dakika ya pili ya mchezo na kuduma mpaka filimbi ya ya mwisho.

Hii ni mara ya pili Algeria wanachukua ubingwa huu, mara ilikuwa ni mwaka 1990 walipomfunga Nigeria bao 1-0 kwenye mchezo fainali ya michuano hiyo iliyofanyika katika ardhi ya Algeria.