Zahera amchagua kocha msaidizi Yanga
Ikiwa mabadiliko katika sekta mbalimbali yanaendelea ndani ya Klabu ya Yanga Mwenyekiti wa klabu hiyo Mshindo Msolla amesema kuwa Kocha mkuu Mwinyi Zahera amemchagua Kocha Noel Mwandila kuwa msaidizi wake kwa kuwa anavigezo vyote vya kuwa katika nafasi hiyo.
Msolla kupitia Clouds FM amesema Kocha Zahera atafanya mabadiliko katika Benchi la ufundi lakini Kocha Mwandila atabaki kuwa msaidizi licha ya hapo awali alikuja yanga kama Kocha wa viungo.

“Kutakuwa na mabadiliko katika Benchi la ufundi lakini mapendekezo ya Kocha kataka Kocha Mwandila aendelee kuwa msaidizi wake kwakuwa leseni ya Mwandila ni kubwa na inamruhusu kuwa Kocha wa mpira wa miguu” Msolla