Mzee Kilomoni amjibu Magori
Baada ya jana uongozi wa Klabu ya Simba kupitia kwa Mkurugenzi wake Crescentius Magori kusema kuwa haimtambui aliyekuwa mdhamini wa Klabu hiyo Mzee Hamisi Kilomoni kama mdhamini ndani ya Klabu hiyo tangu mwaka 2017 walipomvua wadhifa huo,na kuamua kumpeleka kwenye Kamati ya maadili ya TFF na kumshtaki kwa kosa la kupotosha umma kuwa yeye bado ni mdhamini wa Klabu hiyo,Mzee huyo kupitia EFM radio leo amesema kuwa hawamtambui Magori ndani ya Klabu hiyo.
.
“Magori ni nani ndani ya Simba SC ? yeye anazungumza kama nani ndani ya Simba na anacheo gani?” Mzee Kilomoni
Mzee Kilomoni ameongeza kuwa huko alikoshitakiwa kwenye Kamati ya maadili ya TFF ndio atazungumza mambo mengi zaidi.
Kilomoni pia amesema kuwa wiki ijayo siku ya Jumatano atakuwa na mkutano wa mwanzo na mwisho wa kuzungumzia masuala haya.
.
” Wiki ijayo jumatano nitakuwa na mkutano wa mwanzo na mwisho wa kuongelea haya mambo na utakuwa ni wamoto” Kilomoni