Neymar asisitiza kuondoka PSG
Mbrazil Neymar Jr amesisitiza nia yake ya kutaka kuondoka PSG baada ya kufanya kikao kifupi na Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Leonardo, wameripoti ESPN.
Neymar anahusishwa na kutaka kurejea katika timu yake ya zamani ya Barcelona aliyoihama mwaka 2017 na kwenda PSG kutaka kutengeneza ufalme wake.