Tambwe avunja ukimya kwa Zahera
Baada ya mkataba wa aliyekuwa Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Amiss Tambwe kumalizika,mchezaji huyo ameweka wazi kuwa uongozi haukutaka kumuongezea mkataba kutokana na Kocha Zahera kutokumuhitaji.
Tambwe kupitia EFM radio amesema kuwa Kocha mkuu wa Yanga amewaacha wachezaji wengi wazuri lakini hawezi kujua mipango yake ni ipi.
.
“Kama Kocha hakutaki kulingana na mipango yake basi huwezi kumlazimisha maana ni wachezaji wengi wazuri aliowaacha” Tambwe
Tambwe yupo nchini kwao Burundi na mpaka sasa hakuna timu iliyomsajili ingawa kuna timu tayari zimeanza kufanya nae mazungumzo.
.
“Kwa sasa nipo nyumbani na kuna timu zinanihitaji ila mtajua tu ni timu gani nitaenda” Tambwe