TFF yatangaza mrithi wa Amunike
Kocha wa Azam FC Mrundi Etienne Ndayiragije ametangazwa kuwa kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania baada ya kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ya TFF kufanyika jana Julai 11.
Ndayiragije ataanza kazi kwa kutaja kikosi cha wachezaji siku ya jumamosi hii Julai 13 kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu mashindano ya CHAN ambapo Tanzania atakutana na Kenya Julai 28 mwaka huu Kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ndayiragije amependekeza kusaidiwa na Benchi lake la ufundi kwa kumteua kocha wa Coastal Union Juma mgunda pamoja na Kocha Suleiman Matola kutoka Polisi Tanzania.
Kwa upande wa meneja atakuwa aliyekuwa nahodha wa muda mrefu wa klabu ya Yanga na sasa ni meneja wa klabu hiyo,Nadir Haruob Cannavaro na kocha wa makipa ni Salehe Machupa kutoka timu ya Malindi ya Zanzibar.