Koscielny agoma kusafiri na Arsenal
Arsenal wamethibitisha nahodha wao Laurent Koscielny amekataa kusafiri na kikosi kwenda nchini Marekani kwa ajili ya maandilizi ya msimu mpya.
.
“ Tumesikitishwa na vitendo vya Laurent, ambavyo vipo kinyume ya miongozo yetu.
Tunatumaini kutatua tatizo hili na hatutow maelezo yoyote zaidi kwa wakati huu.” Wamesema hivyo Arsenal.
Koscielny,33, yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake Arsenal na anataka kufikia makubaliano na klabu ya kuvunja mkataba.
Mfaransa huyo amepata ofa tatu kutoka Ligue 1 moja ikiwa ya mkataba wa miaka mitatu kutoka Bordeaux na hivyo huo mgomo wake ni wakutaka kulazimisha aondoke.