KMC yashusha kifaa kutoka Rwanda
Klabu ya KMC imemsajili Kiungo Jean Baptise Mugiraneza kutoka katika Klabu ya APR ya nchini Rwanda wa mkataba wa mwaka mmoja.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo umetoa taarifa hiyo kuwa wakiwa nchini Rwanda katika mashindano ya KAGAME CUP mwalimu Jackson Mayanja amevutiwa na kiwango cha kiungo huyo na hivyo kuinasa saini yake.

Kocha Mayanja anaendelea kuimarisha kikosi kwa kuchanganya wachezaji vijana na wenye uzoefu ili kupata uwiano sawa ili kufanya vizuri katika michuano ya Shirikisho la Africa (CAF), TPL pamoja na ASFC.