Nadal na Federer wakutana baada ya miaka 12
Magwiji wawili wa mchezo wa tenesi Roger Federer na Rafa Nadal wanataraji kukutana katika michuano ya Wimbledon kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008 baada ya wote kufuzu hatua ya nusu fainali.
Federer anafika hatua hii baada ya kumtoa Kei Nishikori kwa seti 4-6, 6-1, 6-4, 6-4 huku Nadal akifika hatua hiyo kwa kumfunga Sam Querrey kwa seti 7-5 6-2 6-2 katika mchezo wa robo fainali.
Fainali hiyo ya 2008 waliyokutana, ilichezwa kwa takribani saa 7 baada ya kugubikwa na mvua na kumalizika kwa Nadal kushinda kwa 9-7 katika seti ya 5 .

Fainali hii inatajwa kuwa moja ya mechi nzuri za tenesi kwa muda wote.
Magwiji hao wamekutana mara 39, Nadal ameshinda mara 24 na Federer mara 15 .
Roger Federer ameshinda mataji 8 ya Wimbledon dhidi ya mataji mawili ya Nadal.
Nusu fainali nyingine itakuwa ni kati ya bingwa mtetezi Novak Djokovic dhidi ya Roberto Bautista.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Federer, Nadal na Djokovic wote kufika nusu fainali kwa pamoja baada ya miaka 12.