Dida akubali kucheza daraja la kwanza
Baada ya mkataba wake na Klabu ya Simba SC wa mwaka mmoja kumalizika na kuwa mchezaji huru,kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ amesema kuwa kwa sasa akipata hata timu inayocheza Ligi daraja la kwanza ataenda kucheza.
Dida pia amekanusha taarifa zinazoendelea mtandaoni juu ya yeye kufanya mazungumzo na Klabu ya Coastal Union kwa ajili ya kijiunga na klabu hiyo.