Familia ya Messi yagawa chakula cha bure
Mgahawa unaomilikiwa na familia ya Lionel Messi huko Rosario Argentina, umekuwa ukitoa vyakula vya moto bure kwa wale wenye uhitaji tangu ijumaa iliyopita.
Nchi hiyo ipo katikati ya kipindi cha baridi kwa sasa, hivyo tangu ijumaa mgahawa huo unaoitwa VIP,unawasaidia wasiojiweza kwa kuwapa vyakula hivyo bure na wamepanga kuendelea kufanya hivyo kwa wiki mbili nyingize zaidi mbele.
.
“ Tumekuwa pia tunatoa kahawa, vinywaji laini, na hata pia mvinyo kwa wengine” amesema meneja wa mgahawa Ariel Almada.
.
“Watu wengi wamekuja na wamekuwa wakiheshimu. Tutaendelea kufanya hivi kwa siku 15 zijazo, kila siku usiku kati ya saa moja na saa tatu.”