Lampard arejea darajani kivingine
Frank Lampard ambaye alikuwa kocha wa Derby County ametangazwa kuwa kocha mpya wa Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu.
Lampard ambaye ameitumikia Chelsea kwa miaka mitatu akiwa mchezaji,amejiunga na timu hiyo kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri ambaye ameondoka na kujiunga Juventus.