Maurizio Sarri ampa heshima yake Eden Hazard
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri amekiri kuwa anamshukuru Eden Hazard kwani uwepo uwanjani wake akitokea benchi ulipelekea kuibuka na ushindi katika mechi dhidi ya Crystal Palace jana jumapili.
Muitalia huyo kabla ya mechi alisema kuwa angefanya tendo la ujasiri kumchezesha Hazard ambaye bado anauguza maumivu ya mgongo kama tu angehitajika kwa sababu mchezaji huyo bado hana uwezo wa kucheza dakika zote 90.
Sarri alilazimika kumuingiza Hazard dakika 10 baada ya Andros Townsend kusawazisha goli, na baada ya kuingia akatengeneza goli ambalo lilifungwa na Alvaro Morata, likiwa ni goli lake la pili kwenye mchezo huo.
Pedro akaongeza goli lingine dakika tano baadae kuhakikisha ushindi kwa wana darajani, lakini kocha huyo wa Chelsea sifa zote alizielekeza kwa Eden Hazard ambaye alionekana kubadilisha mchezo wote.
‘ Katika ule wakati ninafikiri tulimuhitaji Hazard matokeo yalipokuwa 1-1 ‘, Sarri aliimbia Sky Sports baada ya mechi kumalizika .
‘ Tulikuwa kwenye matatizo kidogo. Tulihitaji kuongeza kasi , tulihitaji pasi za mabao na Hazard ninadhani alitoa pasi ya goli katika dakika yake ya kwanza uwanjani.
‘Kama nilivyosema kabla ya mechi, ilikuwa ni muhimu sana kuwa nae katika benchi leo ‘
Ushindi wa jana unaifanya Chelsea kufikisha mechi 11 bila kupoteza msimu huu katika ligi kuu na kujikusanyia pointi 27 ambazo zinawaweka nafasi ya pili, pointi mbili nyuma ya vinara Man City.