Samatta asema Tanzania bado ina safari ndefu
Baada ya Tanzania kumalizia mchezo wake wa mwisho hapo jana kwenye michuano ya AFCON dhidi ya Algeria ambapo Tanzania ilifungwa goli 3-0,Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amesema kuwa kama timu bado wanasafari ndefu ya kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano mbalimbali.
.
“Bado tunahitaji kujiandaa vizuri sana,maana mapambano bado ni makali,tunatakiwa kujiandaa sana hasa kushindana na timu zenye viwango vikubwa bado tuna Mlima mkubwa wa kupanda” Samatta
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetolewa kwenye michuano hiyo ambayo wameshiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.