Kenya bado nafasi ya kufuzu mtoano AFCON
Baada ya Kenya kupoteza mchezo wa jana kwa bao 3-0 dhidi ya Senegal, Guinea na DR Congo zimefuzu hatua ya mtoano.
Kenya wanasubiri matokeo ya mechi za Benin na Angola leo ili kujua wanatolewa kwenye michuano au wanaendelea.
Kenya wanaweza kufuzu hatua ya mtoano kwa njia ya timu iliyofanya vizuri na kumaliza nafasi ya tatu katika kundi, maombi ya Kenya ni timu za Benin na Angola zisipate pointi katika mechi zao za leo.
Angola watacheza na Mali, huku Benin wakicheza na Cameroon.