Jezi ya KD kustaafishwa Warriors
Makamu Mwenyekiti mwenza wa Warriors Joe Lacob amesema hakuna mchezaji mwingine wa Warriors atakayekuja kuvaa jezi namba 35 iliyokuwa ikivaliwa na Kevin Durant ambaye ameondoka katika timu hiyo baada ya miaka mitatu na kujiunga na Brooklyn Nets.
Katika misimu mitatu aliyokaa katika timu hiyo ya Warriors, Kevin Durant ameshinda ubingwa wa NBA mara mbili huku akichukua tuzo ya MVP wa fainali za NBA mara mbili.