Arsenal watambulisha uzi wao mpya
Arsenal leo wametambulisha jezi zao mpya za nyumbani ambazo watazitumia katika msimu ujao wa 2019/20.
Arsenal wamerejea kufanya kazi na Adidas kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25 kufuatia mkataba wao na Puma kumalizika msimu ulioisha.

Mkataba wao wa Adidas ambao ni wa miaka mitano, una thamani ya Pauni milioni 60 kwa msimu.
Jezi moja inauzwa kwa Pauni 60 (Tsh 174,000) na ile ambayo huvaliwa na wachezaji inauzwa Pauni 100 ( Tsh 290,000).