Manula na Yondani kuwakosa Algeria leo
Kipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa stars’ Aishi Manula na beki Kelvin Yondani hawatakuwa sehemu ya kikosi cha leo kitakachoshuka Dimbani dhidi ya Algeria katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi katika michuano ya AFCON.
Daktari wa Taifa Stars Richard Yomba amesema kuwa hali za wachezaji kiafya ni nzuri isipokuwa Aishi Manula na Kelvin Yondani hawakuwa sehemu ya mazoezi yaliyofanyika jana kutokana na kuumia katika mchezo uliopita waliocheza dhidi ya Kenya.
.