Kevin Durant aondoka Warriors na kutua Nets
Baada ya sintofahamu ya wiki kadhaa juu ya hatma ya nyota wa NBA Kevin Durant atakapochezea msimu ujao,sasa imefika tamati na nyota huyo anatarajiwa kujiunga na timu ya Brookly Nets kwa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Dola Milioni 164 pungufu ya ule wa dola 221 milioni kama angesaini na Warriors mkataba wa miaka mitano.
KD ataungana na Kyrie Irving ambaye nae anajiandaa kujiunga na Nets huku DeAndre Jordan pia akitazamiwa kujiunga nao akitokea New York Knicks.
Kevin Durant anataraji kukosa msimu ujao mzima kufuatia kuumia mguu wake katika Game 5 ya fainali za NBA mwaka huu dhidi ya Raptors.
Kwa sasa GSW inabaki na nyota wake Steph Curry na Draymond Green huku wakitegemea kumpa mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Dola milioni 190 Klay Thomposon anayetarajiwa kuwa nje msimu ujao mzima kutokana na kuwa majeruhi.
Wakati huo huo Warriors wanakaribia kumsaini D’Angelo Russell kutoka Nets kwa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Dola Milioni 117, na pia Warriors wamem-trade Andre Iguodala kwenda Memphis Grizzlies.