Pep Guardiola amshusha Klopp England.
Mabingwa wa nchini England Man City wanaondoka na ushindi katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya watakatifu Southampton na kujikitika na kileleni mwa ligi.
City iliwagharimu dakika sita tu kupata goli lao kwanza ambalo walilipata kupitia kwa beki wa Southampton Wesley Hoedt aliyejifunga kwa kuunganisha krosi nzuri ya Mjerumani Leroy Sane. Dakika sita baade Sergio Kun Aguero akafunga goli la pili la City kwa kuunganisha pasi kutoka kwa Raheem Sterling.
Goli hilo limemfanya Aguero kuwa mchezaji wa tisa kufikisha magoli 150 katika historia ya ligi kuu nchini England.
Aguero akifunga goli lake dakika ya 12, David Silva nae akasubiri dakika sita zipite na kufunga goli la tatu la City, akipokea mpira kutoka kwa Leroy Sane.
Danny Ings akafanikiwa kurudisha goli moja kwa mkwaju wa penati alioupata baada ya kipa wa City Ederson kumuangusha kwenye eneo la hatari.
Raheem Sterling sekunde chache kabla ya mapumziko akipokea mpira kutoka kwa Aguero akaifungia City goli la nne na kuhakikisha ushindi kwa mabingwa hao.
Kipindi cha pili katika dakika ya 67 Raheem Sterling alifunga goli lingine, tena akipokea pasi ya Sergio Aguero.
City licha ya kuwa mbele kwa goli tano bado walionekana kuwa na njaa ya magoli, Leroy Sane akaifungia City goli la sita kunako dakika ya 90 na mechi kumalizika kwa ushindi wa 6-1.
Kikosi cha Pep Guardiola sasa kimeshinda mechi nane kati ya tisa za mwisho walizocheza katika michuano yote, ingawa goli la Ings ni la kwanza kuruhusu katika ligi kwenye mechi sita za mwisho.
Liverpool walikuwa kileleni baada ya sare yao dhidi ya Arsenal siku ya jumamosi, lakini hawajadumu kwa nafasi hiyo zaidi ya saa 24. City wameichukua nafasi yao wakiwa na pointi 29, Chelsea wakiwa nafasi ya pili baada ya jana kushinda 3-1 dhidi ya Crystal Palace na kufiksha pointi 27.
Liverpool sasa wapo nafasi ya tatu na pointi 27, wakizidiwa tofauti ya magoli na Chelsea.
Wakati huo huo,Southampton sasa wamecheza mechi saba katika ligi bila ya ushindi huku wakiwa nafasi ya 16