Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri ambaye yupo nchini Misri, jana ametembelea kambi ya Taifa Stars na kuwatia moyo wachezaji wa timu hiyo huku akiwataka wasikate tamaa.
Nahodha Mbwana Samatta ambaye pia amejenga Kigamboni amemkabidhi DC Sara jezi ya timu ya Genk anayochezea .
DC Sara yupo Misri kuiunga mkono Taifa Stars ambayo itacheza mchezo wake wa mwisho wa makundi kesho Jumatatu dhidi ya Algeria.