TFF yawataka Watanzania kuiunga mkono timu ya Taifa
Baada ya kuwa na maneno ya kuwakatisha tamaa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ baada ya kufungwa goli 2-0 dhidi ya Senegal Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limewataka watanzania kuendelea kuiunga mkono na sio kuivunja moyo timu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa TFF uliopo Ilala Karume Jijini Dar es Salaam msemaji wake Clifford Mario Ndimbo amesema kuwa kumekuwa na maneno mengi haswa kwa watu wenye majina makubwa hapa nchini baada ya mchezo dhidi ya Senegal , hivyo kwa sasa haitakiwi kufanya hivyo kinachopaswa kufanywa ni kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars.
Mechi ijayo Taifa Stars itacheza dhidi ya Kenya Alhamisi hii na mechi ya tatu watacheza dhidi ya Algeria Jumatatu ijayo Julai Mosi.