Simba yashusha Mbrazil mwingine
Klabu ya Simba imemsajili mchezaji anacheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji raia wa Brazil Gerson Fraga Vieira kwa kandarasi ya miaka miwili.
Beki huyo ambaye amewahi kuwa nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil chini ya miaka 17 iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar wa PSG , Philippe Coutinho wa Barcelona, Casemiro wa Real Madrid na golikipa Alisson Becker wa Liverpool.

Kikosi hicho kilishiriki michuano ya kombe la Dunia chini ya miaka 17 iliyofanyika mwaka 2009 nchini Nigeria
Pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20.
Mchezaji huyo amejiunga na Simba akitoka ATK inayoshiriki ligi kuu nchini India.