Curry na Serena washinda BET
Leo katika tuzo za BET nyota wa Golden State Warriors Steph Curry ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume wa mwaka na mcheza Tenesi Serena Williams ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kike wa mwaka.

Hii ni mara ya nne kwa Steph Curry kushinda tuzo hiyo, na ni mara ya 13 kwa upande wa Serena.