Hamilton aendelea kutesa Formular 1
Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton ameendeleza ushindi wake katika Formular 1, leo ameibuka mshindi wa French Grand Prix huku dereva mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas akishika namba mbili na Charles Leclerc wa Ferrari akimaliza namba tatu.
Huu ni ushindi wa 6 wa Hamilton katika mbio nane za mwaka huu, na pia ni ushindi wake wa nne mfululizo.
Muingereza huyo anaendelea kushika usukani katika msimamo wa madereva msimu huu akiwa na jumla ya pointi 187 na nafasi ya pili ikishikwa na dereva mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas mwenye pointi 151.