Chirwa apewa mkataba Azam FC
Baada ya makubaliano ya pande zote mbili, mshambuliaji Obrey Chirwa amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia klabu ya Azam.
Mzambia huyo ambaye alijiunga na Azam FC Novemba mwaka jana kwa mkataba wa muda mfupi, alikuwa ni miongoni mwa wachezaji nane waliotangazwa kuachwa na timu hiyo Jumanne hii.