Ferrari waulilia ushindi wa Vettel wa Canada
Baada dereva Sebastian Vettel wa Ferrari kupokwa ushindi kwa kupigwa penati katika mbio za Canada GP Juni 9 mwaka huu, timu yake ya Ferrari itawasilisha ushahidi mwingine hapo kesho Ijumaa katika mbio za French GP kwa wasimamizi ili uamuzi huo kupitiwa upya.
Upande wa pili dereva wa timu ya RedBull Max Verstapen aliyemaliza katika nafasi ya tano kwenye mbio hizo, akihojiwa na kituo cha Sky Sports ameonyesha wazi kutoridhishwa na uamuzi huo na kusema zinaharibu sura ya mchezo huo wa mbio za Formular 1.
Katika mbio hizo za Canada, Vettel alipaliza wa kwanza lakini ushindi akapewa Lewis Hamilton ambaye alimaliza wapili, kufuatia Vettel kupigwa penati ya sekunde 5 kwa kosa la kujiunga tena na barabara kwa njia isiyo sahihi.