Taifa Stars yachangiwa Milioni 370
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars imechangiwa Tsh shilingi million 370 katika harambee iliyozinduliwa leo na kuongozwa na makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
.
Harambee hiyo imefanyika leo katika moja ya ukumbi uliopo katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam.
.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Kampeni hii ni endelevu na ana matumaini kupitia mikoani pamoja na makampuni mengine yakichangia wataweza kufika mbali zaidi kuendelea kuichangia timu ya Taifa.
.
” Makampuni mengi yameahidi kuchangia kwa hatua, na makampuni mengi yamejitolea kuchangia kwa hatua hivyo timu yetu ikifika robo fainali tutakuwa na michango mingine ambayo tutakwenda vizuri.” ameasema Makamu wa Rais,Samia
Pesa hizo zitaendelea kuisaidia Taifa Stars ambayo ipo nchini kwa ajili ya michuano ya AFCON inayotarajiwa kuanza Juni 21 mwaka huu.