Paul Makonda atoa Hekari 15 kwa Taifa Stars
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametoa Uwanja wa Hekari 15 kwa Taifa Stars chini ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kwa ajili ya kujenga kituo/shule ya soka ‘Soccer technical Center’ ili kuendelea kuendeleza vipaji kwa vijana na kupata wachezaji wazuri katika timu ya taifa.
Makonda amesema kuwa kesho atakapoenda kuwakabidhi Yanga eneo alilowapatia lililopo Kigamboni pia atatumia nafasi hiyo kuwaonyesha TFF eneo hilo.
Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji ya Taifa Stars, ameyasema hayo leo katika harambee ya kuchangia timu hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.