Sarri kumfuata Ronaldo Ugiriki
Baada ya kutua mjini Turin jana na kuwasili rasmi katika klabu ya Juventus, kocha Maurizio Sarri ameripotiwa kuwa anajiandaa kumfuata nyota wa timu hiyo Cristiano Ronaldo nchini Ugiriki ambapo ameenda na familia yake kula likizo.
Sarri anataraji kutambulishwa rasmi kama kocha mpya wa Juventus leo, na kwa mujibu wa gazeti la Corriere dello Sport la nchini Italia, kocha huyo baada ya utambulisho huo atapaa kuelekea Ugiriki kuonana na Ronaldo kwa ajili ya kuzungumza kuhusu mipango ya msimu ujao.
Cristiano Ronaldo yupo nchini ugiriki na mpenzi wake Georgina Rodriguez pamoja na mtoto wake Cristiano Ronaldo Jr.