Ambokile atua TP Mazembe
Aliyekuwa Mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile amejiunga na Klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Imeripotiwa kuwa amesajiliwa kwa ada ya milioni 50.
.
“Nimesaini jana mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea TP Mazembe na hivi sasa nipo Congo kwa ajili ya kuweka mambo sawa” Ambokile ameiambia Worldsports14
.
Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu Ambokile alikwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio katika timu ya Black Leopard lakini hakufanikiwa kusaini nao mkataba, na kabla ya kwenda kwenye majaribio hayo, alikuwa ni moja ya mchezaji wenye magoli mengi katika ligi kuu Tanzania bara akiwa na magoli 10.