Enrique aachana na Hispania
Rais wa Shirikisho la soka la Hispania,Luis Rubiales leo ametangaza kuwa kocha Luis Enrique hataendelea kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Hispania na nafasi yake itachukuliwa na kocha wake msaidizi, Robert Moreno.
Moreno ambaye nae ni Mhispania, ameanza kufanya kazi na Luis Enrique tangu wakutane katika kikosi cha Barcelona B, wakaenda kufundisha wote AS Roma, Celta Vigo, Barcelona mpaka kwenye timu ya Taifa ya Hispania.
Moreno ndiye aliyeiongoza Hispania katika michezo mitatu iliyopita dhidi ya Malta, Faroe Islands na Sweden na kufanikiwa kushinda yote.
Luis Enrique hajaifundisha timu hiyo tangu mwezi Machi mwaka huu kufuatia kuwa na matatizo binafsi yanayomkabili, na sasa wameamua kumpa kibarua Moreno moja kwa moja.
Luis Enrique ameifundisha timu ya Taifa ya Hispania kwa muda wa miezi 11 tu.