Henry bado hajaisaidia AS Monaco
Kocha mpya wa AS Monaco ambaye amewahi kuichezea klabu ya Arsenal, Thierry Henry anadaiwa kuanza kuwa katika hali ya presha kutokana na timu yake ya AS Monaco kuzidi kuboronga katika michezo ya Ligi Kuu Ufaransa msimu wa 2018/2019.
Henry anadaiwa kuanza kuwa na hofu ya kibarua chake kutokana na kuiongoza AS Monaco katika mechi nne lakini hakuna hata mchezo mmoja ulioshinda akiiongoza timu hiyo na imezidi kuwa katika nafasi za hatari za kushuka daraja japo Ligi bado mbichi.
Kipigo cha goli 1-0 ambalo limefungwa na Mathieu Cafaro dakika ya 24 , limeipa alama tatu Reims na kuifanya AS Monaco izidi kudidimia na kuzidisha hofu kubwa kwa mashabiki wa Monaco juu ya mwenendo wake.
Hadi sasa AS Monaco ipo nafasi ya 19 ikiwa nafasi ya pili kutoka mwisho katika Ligi Kuu ya Ufaransa ikicheza michezo 12, imeshinda mchezo mmoja, sare michezo minne na imepoteza michezo saba, imeshinda magoli 12 msimu huu na kuruhusu kufungwa magoli 18.