Mwantika arejeshwa Taifa Stars
Beki David Mwantika amerejeshwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kuchukua nafasi ya beki mwenzake wa Azam FC, Agrey Morris ambaye aliumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri uliopigwa wiki jana.
Mwantika alikuwa ni miongoni mwa wachezaji 9 walioachwa katika mchujo wa mwisho wa kikosi cha AFCON 2019 cha Taifa Stars chini ya kocha Mnigeria Emmanuel Amunike.