Paul Scholes apigwa faini kwa ku-bet
Kiungo wa zamani wa Man United Paul Scholes amepigwa faini ya Pauni 8,000 (Tsh Milioni 23) kwa ku-beti katika mechi za mpira wa miguu kati ya mwaka 2015 na 2019 wakati akiwa sehemu ya wamiliki klabu ya Salford City.
Scholes amepigwa faini hiyo na chama cha soka cha England FA leo Jumatano kwa kuweka jumla ya bet 140 katika kipindi hicho cha miaka minne.
Kiungo huyo wa zamani ameomba msamaha kwa kosa hilo leo akisema : Ninakubaliana na utawala. Ningependa kuomba msamaha na ninaelewa na kukubali faini niliyotozwa na FA”
.
Scholes amesema kuwa alikuwa na imani mbaya ya kuamini kuwa, kwa vile hakuna mahusiano yoyote binafsi na mechi alizokuwa anazifanyia ubashiri hivyo hakukuwa na tatizo lolote.
Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuwa Scholes alikuwa akifanya ubashiri wa matokeo ya mechi za Salford City.
Bet 8 alizoweka zilikuwa zinahusiana na Man United, na kipindi hicho Ryan Giggs na Nicky Butt ambao ni watu wake wa karibu walikuwa wakifanya kazi katika timu hiyo, na Bet nyingine ilikuwa ni Valencia kuifunga Barcelona, ambayo aliiweka wakati Gary Neville na Phil Neville wakiwa wanafanya kazi Valencia.
Mwaka 2014 FA walizikaza sheria za michezo ya kubashiri, ambapo ilikataza mtu yoyote anayehusukia katika timu kwenye ngazi zote za mpira wa miguu asishiriki kucheza michezo ya kubashiri katika mchezo huo wa mpira wa miguu.