Chirwa na wenzake 7 watemwa Azam FC
Klabu ya Azam FC imeachana na wachezaji wake nane baada ya mikataba yako kuisha na sasa wachezaji hao ni wachezaji huru.
Wachezaji hao ni Obrey chirwa ,Daniel Lyanga,Joseph kimwaga,Enock Atta,Ramadhani Singano,tafadzwa Kutinyu,Steven Kingu na Hassan Mwasapili
Msemaji wa Klabu hiyo Jaffar Iddi Maganga amesema kuwa uongozi wa juu tayari umeishafanya mazungumzo na wachezaji hao na umeishawapa ruhusa ya kuangalia timu zingine.
.
“Uongozi wa juu leo umenipatia majina ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika na hawawezi kuendelea na Azam FC, na wachezaji hawa walikuwa na mkataba hadi msimu uliopita ukamalizika na sasa hatutaweza kuendelea nao na uongozi wa juu umefanya mazungumzo na wachezaji hao na imetoa ruhusa ya kuweza kutafuta maisha ya Soka katika timu nyingine.” Msemaji huyo Jaffary Maganga ameviambia vyombo vya habari leo.
Maganga ameongeza kuwa kwa niaba ya Azam FC inawashukuru wachezaji hao kwa mchango wao mkubwa walioutoa ndani ya Klabu hiyo na wanaimani watafanya vizuri huko waendako.